Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa jana aliwatembelea wahanga waliookolewa mgodini baada ya kunasa kwa siku 41 waliolazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Lowassa ambaye aliambatana na mbunge wa viti maalum (Chadema) mkoa wa Shinyanga, Bi. Salome Makamba alitoa mchango wa shilingi 2,000 kwa wahanga hao wanne ambapo kila mmoja alipata shiilingi 500,000.

Joseph Burule mmoja kati ya wahanga hao alimshukuru Lowassa kwa ujio wake na kueleza kuwa licha ya kuwa wamefarijika sana kumuona lakini pia amewakumbusha kifo cha mhanga mwenzao aliyefariki juzi mchana.

Burule alisema kuwa wamefarijika kumuona Lowassa akiwapa pole na kwani tangu walazwe katika hospitali hiyo hakuna kiongozi yoyote wa serikali ngazi ya taifa aliyefika kuwapa pole mbali na viongozi wa wilaya ya Kahama.

Aidha, wahanga hao walitumia nafasi hiyo kuomba wahusika wafanye utaratibu wa kuwahamishia katika hospitali ya Bugando ili waweze kupata uchunguzi zaidi na kueleza kuwa kifo cha mwenzao kiliwaongeza hofu na kuona kuwa wao pia wanaweza kupoteza uhai muda wowote kwani walikuwa wanaongea naye na kutaniana kuhusu kilichowasibu kabla hajapoteza maisha.

Lowassa Geita

Wananchi wengi walifika katika hospitali hiyo kumuangalia Lowassa na walianza kuimba na kumshangilia kabla ya Mbunge wa viti maalum wa Chadema, Bi. Salome Makamba kuwasihi wasishangilie katika eneo la hospitali huku akiwaahidi kuwa Lowassa angezungumza nao nje ya hospitali hiyo ili kuepusha kuwasumbua wagonjwa.

Hata hivyo, Lowassa hakuzungumza chochote katika hospitali hiyo mbali na kuwapa pole wahanga hao na kuwapa pole. Alipotoa nje aliwaaga wananchi hao na kurejea jijini Mwanza alikotokea.

 

 

Wafanyakazi Wa Maduka Ya Uchumi Supermarket Walalamikia Kuzulumiwa Stahiki Zao
Kesi ya Kumuaga Mawazo wa Chadema Kuunguruma Leo