Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imepokea vielelezo vya shahidi wa tisa wa upande wa Jamhuri, Marry Mayoka Kimasa chini ya Kifungu cha sheria ya ushahidi namba 78 na 79, huku nyaraka ya leseni ikikataliwa kupokelewa kwa kukosa uthibitisho wa mwanasheria.

Novemba 16,2021 vielelezo hivyo vilipingwa na mawakili wa upande wa utetezi kwa kuainisha makosa ya uwasilishwaji wake na kupelekea mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi leo ambapo mahakama imetoa uamuzi juu ya pingamizi hilo.

Vielelezo hivyo ni barua mbili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na ya kuamuru kutoa nyaraka mbalimbali kama ‘Bank statement’ ya Francis Mroso, ‘withdraw slip’ ya Mroso ya tarehe 22.1.2021 ‘mandet file’ inayoonyesha mmiliki wa akaunti hiyo ambaye alikuwa Fransic Mroso pamoja na CCTV video za tarehe 22.1.2021.

Mkuu wa magereza afutwa kazi baada ya wafungwa 3 kutoroka - Kenya
Waziri Ummy: Tegemeeni makubwa ujenzi wa barabara za vijijini