Kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane amewaonya Kaizer chiefs kuelekea mchezo wa fainali wa ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF) kuwa watahitaji pumziko la nguvu baada ya mchezo.

Al Ahly na Kaizer chief watakutana kwenye fainali itakayochezwa kwenye uwanja wa Stade Mohamed V huko Casablanca nchini Morocco Jumamosi Julai 17.

Mosimane ana wasiwasi timu yake inaweza kuwa katika hali ya uchovu, ikizingatiwa bado hawajamaliza msimu kwenye ligi yao ya ndani ambapo watakuwa na michezo mitatu itakayochezwa Julai 4, 8 na 11.

Kwa upande wa Kaizer wao, wana shida tofauti wamekuwa hawachezi mchezo wowote tangu mkondo wa pili wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Wydad Casablanca zaidi ya wiki mbili zilizopita.

“Sijui kama ni faida au hasara. Ikiwa unasema ni faida kwa Ahly, basi Kaizer Chiefs hawachezi na hawana majeraha , “

“Unaweza kusema ni hasara kwetu, tunaweza kupata majeraha na uchovu uliozidi kutokana kwa michezo mingi kwenye ligi ya Misri ni ngumu sana. “

TFF yalaani kauli ya Waziri Bashe
TFF yamshukuru Rais Samia