Shirikisho la soka nchini TFF limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaongoza mashabiki waliojitokeza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba SC dhidi ya Young Africans.

Rais Samia alifika uwanajni hapo kwa kushtukiza, hali ambayo ilileta mshangao kwa mashabiki waliokua wamejitokeza kwa wingi uwanjani hapo.

TFF kupitia taarifa yake iliotoka jioni hii, inaamini kitendo cha Rais Samia kufika uwanjani jana Jumamosi (Julai 03), kimedhihirisha yeye ni mwanamichezo hususan mpira wa miguu.

Katika mchezo huo Simba SC ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Young Africans, bao likifungwa na kiungo Zawadi Mauya.

Ushindi huo umeiwezesha Young Africans kufikisha alama 70 zinazoiweka timu hiyo katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba SC yenye alama 73 inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu, na Julai 07 itacheza dhidi ya KMC FC jijini Dar es salaam.

Pitso Mosimane aihofia Kaizer Chiefs
UEFA yamaliza utata ufungaji bora Euro 2020