Wakati michuano ya Euro ikisubiriwa kupigwa michezo miwili ya nusu fainali siku ya Jumanne na Jumatano jina la mkali wa kufumania nyavu Christiano Ronaldo linaendelea kuzungumzwa, Barani Ulaya na kwingineko duniani.

Hayo yanatokana na shirikisho la soka Barani Ulaya (UEFA) kuweka wazi sababu za Ronaldo kuendelea kuongoza kwenye orodha ya upachikaji mabao kunako michuano hiyo akiwa na mabao matano licha ya kuwa sawa na mshumbulizi wa Jamhuri ya Czech Patrik Schick

Kwa mujibu wa UEFA Ronaldo ana faida ya kutoa assist kwa Diogo Jota kwenye kipigo cha mabao manne kwa mawili dhidi ya Ujerumani katika hatua ya 16 bora

Mbali na wakali hao wengine ni Benzema mwenye mabao manne sambamba na Romelu Lukaku huku pia Emil Forsberg wa Sweden naye akiwa na kamba nne.

TFF yamshukuru Rais Samia
Waziri Aweso: Sishindwi kuwachukulia hatua