Kocha wa timu Yanga, Hans Van Pluijm amesema ni mapema sana kusema Yanga itatwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Tanzania Bara licha ya kuwafunga watani wao, Simba SC mabao 2-0.

Yanga ilifanikiwa kuishusha Simba SC kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu mara baada ya kufikisha pointi 46 baada ya kushuka dimbani kwenye michezo 19 huku ikiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Yanga ipo kileleni mwa msimamo wakipumuliwa kwa ukaribu na Azam FC yenye pointi 45 baada ya kushuka dimbani mara 18 mchezo mmoja pungufu dhidi ya Yanga.

Mbali na Azam timu nyingine yenye nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo ni Simba SC yenye pointi 45 ikiwa nafasi ya tatu kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Mayanja Afafanua Kwa Nini Simba Walipokea Kibano
Yanga Kuwavaa Maafande Wa JKT Mlale Jumatano