Polisi wa Marekani walivamia katika jumba la kifahari la msanii wa Nigeria, Davido lililoko Atlanta, Georgia nchini humo.

Davido aliweka wazi taarifa hizo hivi karibuni alipofanya mahojiano na Jarida la Marekani la Fader, akidai kuwa tukio hilo lilitokea mwaka jana aliponunua jumba hilo karibu na jumba la rapa Future.

Davido 2

Davido anasema kuwa majirani zake walishtuka kuona mtu wa Afrika akinunua nyumba tena kwa fedha taslimu katika eneo hilo la matajiri, hivyo walianza kumhisi kuwa anafanya biashara haramu ya dawa za kulevya na kuwasilisha hisia zao kimyakimya kwa jeshi la polisi.

“Nahisi lazima kuna jirani alijaribu kuni-snitch. Waliniona na kufikiria, ‘huyu Mu-Afrika ameingiaje hapa,?”Davido alisimulia.

Anasema baada ya jeshi la polisi kufika katika eneo hilo, alipata wakati mgumu awali kuwaeleza kuwa yeye ni mtu maarufu Afrika wakati wao walionesha kutomfahamu hata kidogo. Hivyo, aliamua kuingia YouTube na kuwaonesha kazi zake pamoja na mamilioni ya watu wanaozifuatilia.

“Nawezaje kumwaminisha mtu ambaye hajawahi hata kunisikia, kuwa mimi ni maarufu. Niliwaonesha videos zangu YouTube. Walizipenda,” Davido aliliambia jarida hilo.

 

BBC: Guardiola Hawezi Kuchomoka Man City
Wachezaji Wa Azam FC Kupumzika Kwa Siku Kadhaa