Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma, kwa kushirikiana na Wananchi wa Kijiji cha Kandaga wamefukua kaburi la mtu mmoja, Henry James aliyedaiwa kufariki mwezi April, 2022 na kisha kupatikana akiwa hai mwaka jana (Desemba, 2022).

Tukio hilo ambalo limefanyika Wilayani Uvinza, limefanyika mbele ya Wataalamu wa Afya waliochukua sampuli za vipimo katika mwili huo, ambazo zitapelekewa kwa Mkemi Mkuu wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi wa vinasaba.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, Filemon Makungu.

April 19, 2022, ilitokea ajali ya gari kugonga mtu eneo la Mazungwe Wilayani Uvinza ambapo ndugu wa marehemu walifika na kumtambua mpendwa wao na kisha taratibu za mazishi zilifanyika baada ya Polisi kuwakabidhi mwili.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma, Filemon Makungu alisema mtu huyo anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili, atafanyiwa uchunguzi wa kisayansi ili kujua ukweli wa aliyefariki na aliyepatikana akiwa hai.

Thierry Henry: Ten Hag ana mwaka mmoja Man Utd
Azam FC yafichua alipo Tape Edinho