Jeshi la Polisi jana lilifanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyekuwa na kilo 22 za dawa za kulevya aina ya mirungi akiisafirisha kuelekea Uingereza kupitia Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.

Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa viwanja vya ndege, Martin Otieno aliyemtaja mtuhumiwa kwa jina la Faiz Abdullah, raia wa Uingereza mwenye asili ya Somalia, alisema kuwa alikuwa ameiweka mirungi hiyo kwenye mabegi mawili huku akiwa ameifunga ndani ya khanga ili mashine zisiweze kutambua alichobeba.

“Lakini kwa sababu mashine zetu ni za kisasa ziliweza kuonesha kuwa kilichomo ndani ni mirungi, “alisema Kamanda Otieno.

Kamanda Otieno alieleza kuwa mtuhumiwa alipanga kusafirisha mirungi hiyo kwa ndege ya Shirika la Emirates na kwamba alipohojiwa alidai kuwa aliingia nchini kufanya utalii.

 

Aliyeokolewa Mgodini Baada Ya Siku 41 Afariki
Magufuli awatoa sakafuni wagonjwa 300 Muhimbili