Mmoja kati ya wahanga watano waliookolewa wakiwa wamenasa ndani ya shimo la mgodi kwa siku 41 wilayani Kahama mkoani Shinyanga amefariki dunia.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Kahama, Joseph Ngowi alimtaja marehemu kuwa ni Onyiwa Kaiwao mwenye umri wa miaka 55.

Dkt. Ngowi alieleza kuwa mgonjwa huyo alifikwa na umauti baada ya matapishi kupitia katika njia ya hewa (suffocate). Alieleza kuwa mgonjwa huyo pia alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa nimonia unaotokana na baridi kali, hivyo hali yake ilikuwa mbaya zaidi tofauti na wenzake.

“[juzi] tuliwachukua vipimo waathirika wote watano na kuonesha kuwa hali zao ni nzuri, lakini Onyiwa alionesha kutokuwa na maendeleo mazuri tofauti na wenzake na ghafla akiwa amelala alijitapikia hali ambayo matapishi hayo yaliingia katika mirija ya hewa na kuziba hali iliyosababisha kifo chake,” alisema Dkt Ngowi.

Alieleza kuwa wagonjwa wengine wanaendelea vizuri na kwamba wanapata matibabu ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi huku hospitali hiyo ikiwa imechukua tahadhari ya kuwahamishia katika hospitali ya Rufaa endapo hali yao itabadilika.

 

 

Albam Mpya ya Adele '25' Kuweka Historia Kubwa ya Mauzo
Polisi wanasa dawa za kulevya Uwanja wa Ndege