Albam mpya ya Adele ‘25’ inatarajiwa kuweka historia mpya ya rekodi kubwa zaidi ya mauzo ya albam katika wiki ya kwanza sokoni.

Bilboard wametabiri kuwa Adele anaweza kuuza nakala zaidi ya milioni 2.5 za CD pekee ndani ya wiki moja na kuvunja rekodi iliyowekwa na NSYNC ya ‘No Strings Attached’.

Hakuna albam ya mwanamuziki yeyote baada ya ‘No String Attached’ ya NSYNC iliyowahi kuuza nakala milioni 2 ndani ya wiki moja tangu kampuni ya Nelsen Music kuanza kufuatilia taarifa ya mauzo ya albam mwaka 1991. Hivyo, mauzo ya ‘25’ ya Adele yataweka historia kubwa.

Albam hiyo itapatikana kwa njia na CD na iTunes pekee.

 

 

Mtanzania Ashinda Tuzo Ya Mfanyabiashara Bora Kijana Afrika
Aliyeokolewa Mgodini Baada Ya Siku 41 Afariki