Mfanyabiashara wa kitanzania, Edha Nahidi ameshinda tuzo ya mfanyabiashara bora kijana barani Afrika katika tuzo za ‘All Africa Business Leader Awards (AABLA 2015)’ iliyotolewa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Sandton, Afrika Kusini.

Edha ambaye pia ni Mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Amsons Group alishinda tuzo hiyo ya Vinara wa Biashara Afrika za mwaka 2015 (AABLA 2015) inayotolewa kwa ushirikiano na CNBC Afrika akiibuka kuwa mfanyabiashara bora zaidi kijana wa mwaka (Young Business Leader of the Year) akiwashinda washiriki wenzake kutoka pande zote za bara la Afrika.

Alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo baada ya mchakato wa kuwachuja washiriki waliokusanyika kutoka sehemu mbalimbali na kuonesha bidhaa zao na kutambua mchango wao katika sekta ya viwanda.

Utata Watawala Kifo cha Ghafla Cha Msemaji Wa Madereva, Rashid Saleh
Albam Mpya ya Adele '25' Kuweka Historia Kubwa ya Mauzo