Polisi nchini Uganda, wametangaza kusitishwa mara moja kwa kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji iliyokuwa ikiendeshwa na chama kikuu cha upinzani kinachoongozwa na Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.
Polisi wameeleza kuwa, katika maeneo yote kulikofanyika shughuli hizo za uhamasishaji, kulishuhudiwa vitendo vya uvunjifu wa usalama, fujo, foleni zisizo za lazima, kupungua kwa shughuli za kibiashara na uharibifu wa mali.
Hatu hiyo ni kutokana na kile Polisi wamesema ni makosa ya kumkashifu rais na kuvuruga usalama wa umma.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP Bobi Wine ameliambia shirika hilo kuwa harakati hizo zitaendelea kote nchini na Jumatano hii walikuwa huko Arua kaskazini magharibi mwa Uganda.
Jukwaa hilo la Umoja wa Kitaifa lilipewa idhini rasmi kwa operesheni hiyo iliyozinduliwa Septemba 2, hatua ambayo ni nadra katika nchi ambayo vyama vya upinzani vimekuwa chini ya udhibiti mkali wa Rais Yoweri Museveni tangu mwaka 1986.