Ndugu wanne wa Familia moja, wamefariki baada ya gari aina ya Toyota Prado walilokuwa wakisafiria kutokea Dar es salaam kwenda Same Mkoani Kilimanjaro kugongana uso kwa uso na Lori aina ya Scania lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Piusi Lutumo amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo Agosti 3, 2023 eneo la Mapatano lililopo Kata ya Mbwewe Chalinze.

Amesema, waliofariki ni Dereva wa gari Nechi Msuya (45-50), Mkurugenzi wa Benki ya APSA na Mkazi wa Dar es salaam pamoja na Watu watatu waliokuwa kwenye gari hilo ambao ni Dayana Mageta(40-45), Norah Msuya (40-45) na Ndugu mwingine wa kike.

Aidha, Kamanda Lutumo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Prado ambaye alihama upande wake na kugongana uso kwa uso na Scania huku miili ya marehemu wote ikiwa imehifadhiwa katika Zahanati ya Lugoba.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Agosti 4, 2023
Kassongo aikubali Dar24 Media kutwaa Tuzo saba EJAT