Baadhi ya Wanaume wanaopitia adha ya ukatili katika ndoa ikiwemo kupigwa na kunyimwa unyumba na wenza wao, huku wakiona aibu kufika kituo cha Polisi kuripoti ukatili huo wametakiwa kuripoti matukio hayo bila woga ili kupata msaada.

Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Mkoani Iringa, Lydia Sospeter hii leo Januari 23, 2023 ambaye amesema Wanaume hao hufanyiwa ukatili na kushindwa kuripoti katika dawati kitu ambacho kinaweza kuwasababishia matatizo, ikiwemo kifo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi.

Amesema, “mtakufa na tai shingoni mnaona aibu mwishoni mnaamua kujinyonga msikae kimya njooeni mripoti katika dawati ili hatua stahiki zichukuliwe msikae kimya pale mnapotendewa ukatili madhara yake ni makubwa.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoani Iringa, Elizabeth Swai amewaasa wanafunzi kutoa taarifa kwa Polisi, endapo wataona wapo katika mazingira hatarishi na yenye viashiria vya ukatili wa kijinsia ili kupatiwa msaada stahiki.

ADF wadaiwa kuuwa raia 28 kwa mapanga
Mpenzi ataka turudiane akiwa na mimba ya mwanaume mwingine, nifanyaje?