Kikundi cha watu wenye silaha kimevamia makazi ya muda ya raia mtaa wa Umlazi uliopo karibu na mji wa Durban ulioko kusini mashariki mwa Afrika Kusini na kuwauwa watu wanane na kuwajeruhi wengine wawili.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi nchini humo imeeleza kuwa, mashambulio ya ufyatuaji wa risasi nchini humo yamekuwa yakishamiri na kwamba watu saba walifariki papo hapo na mtu wa nane alifariki siku moja baadaye.

Polisi imesema wanaume 12 walikuwa ndani ya chumba kimoja wakinywa pombe na ghafla watu hao wenye silaha waliwavamia na kuwapiga risasi na kisha kukimbia.

Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi 10 zenye idadi kubwa ya matukio ya mauaji ya kukusudia duniani na katika miaka ya hivi karibuni nchi hiyo imekuwa ikiripoti visa vingi vya mashambulizi ya risasi yanayowalenga watu wengi.

Andy Cole: Man Utd bado sana kutwaa ubingwa
DP Word kuleta mageuzi makubwa bandari ya Dar es Salaam