Mwana mfalme wa Uingereza, Harry ametangazwa kuwa Mshindi wa Peoples Magazine kwenye kipengele cha Mwana mfalme mwenye mvuto zaidi Duniani, ambaye bado anaishi, akiwashinda wenzake kibao akiwemo kaka yake Prince William.

Harry anashinda nafasi hii ukiwa umepita mwaka mmoja tu, tangu alipotangazwa kuwa ni Baba mwenye mvuto zaidi kati ya mababa wote wenye watoto Duniani.

Mshiriki ambaye alikuwa anamkaribia na alikuwa mpinzani wake wa karibu ni Prince Carl Philiph (41), kutoka Nchini Sweden.

Miongoni mwa mambo yanayoendelea kumpa umaarufu zaidi Prince Harry, ni uamuzi wake wa kuondoka kwenye jumba la Kifalme Uingereza na kwenda kuishi Marekani na mkewe Meghan.

Rais Mwinyi awaapisha Mawaziri, awaagiza kuanza na hili
Trump kushiriki mkutano wa G20

Comments

comments