Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu ameongoza kikao cha majadiliano kati ya ofisi hiyo na Wizara ya Kazi nchini Kenya kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhamaji nguvu kazi, ukuzaji ujuzi kwa vijana, ukuzaji ajira na masuala mengineyo yanayohusu sekta ya kazi na ajira.

Akizungumza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Katundu amesema kikao hicho cha majadiliano kitafungua fursa kwa nchi hizo kushirikiana kwa karibu katika kubadilishana uzoefu juu ya  utekelezaji wa  majukumu sambamba na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu akiongoza kikao cha majadiliano kati ya ofisi hiyo na Wizara ya Kazi nchini Kenya walipotembelea Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko amepongeza namna ambavyo Ofisi ya Waziri Mkuu katika kukuza fursa za ajira, viwango vya kazi sambamba na kusimamia usalama na afya kwa wafanyakazi.

Aidha, Ujumbe huo umetembelea ofisi za Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) pamoja na Kitengo cha Huduma za Ajira (TaESA), na ugeni huo umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi nchini Kenya, Bw. Geoffrey Kaituko  anayesimamia masuala ya Kazi nchini Kenya. 

Simba SC, Young Africans zaingiza Milioni 400
Mayele, Musonda wakabidhiwa kazi maalum