Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, ameonesha kushangazwa na utaratibu uliotumika kuwashughulikia watu waliotuhumiwa kuchota shilingi bilioni 306 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, yeye akiwa mmoja kati ya watuhumiwa hao.

Profesa Tibaijuka aliondolewa katika nafasi ya Uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika Serikali ya Awamu ya Nne, baada ya kutuhumiwa kupokea mgao wa fedha hizo kupitia Benki ya Mkombozi.

Akizungumza katika Semina maalum iliyoandaliwa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Ufisadi (ACFE), kwa lengo la kuwajengea uwezo wabunge kupambana na ufisadi, Profesa Tibaijuka alisema kuwa anashangaa yeye alituhumiwa kupokea fedha lakini aliyempa fedha hakuguswa.

Aidha, Profesa Tibaijuka alisema kuwa ingawa fedha hizo zilitolewa kupitia Benki mbili tofauti (Stanbic Bank na Mkombozi Bank), watuhumiwa waliotoa pesa Mkombozi Bank ndio walianikwa huku majina ya waliochukua fedha kupitia Stanbic yakigeuka siri.

Mbunge huyo alionesha kutokuwa na imani na Tume ya Maadili inayohoji watuhumiwa wa masakata ya Ufisadi akidai kuwa haiko makini kwani kuna watuhumiwa wengine ambao hawakutajwa Bungeni hawakugushwa na Tume hiyo.

“Mie nimeshawahi kushtakiwa Tume ya Maadili, najua kuwa kuna mbunge mwenzetu hapa alipata fedha za Escrow, lakini kwa sababu hakuwa mzungumzaji ameondoka bungeni wala hakuna mtu anajua kama alipata. Unaona jinsi ambavyo hawa watu hawako makini,” alisema.

Profesa Tibaijuka aliinyooshea mkono Takukuru akidai kuwa imekuwa ikichagua kesi za rushwa na ufisadi inapotaka kufanya uchunguzi.

Video Mpya: Rich Mavoko - Ibaki Story
Besiktas Wasisitiza Mazungumzo Ya Usajili Wa Martin Skrtel