Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameibuka mshindi kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine ujao wa miaka sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa.
Ushindi huo ulitarajiwa katika upigaji kura uliomalizika siku ya jumapili hata kabla ya kura zote kuhesabiwa tayari alikuwa amejizolea asilimia 76 kwa mjibu wa tume ya uchaguzi.
Akizungumza katika mkutano wa kutangazwa mshindi amesema ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake.
Amesema kuwa hii ni uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake na kwamba hana mpango wowote wa kufanya marekebisho ya katiba na kusisitiza umoja na mshikamano.
“Hadi hapa sina mpango wowote wa kufanya marekebisho yoyote ya Katiba, kuhusiana na uenyekiti na serikali kwa ujumla. nilikwisha sema awali kwamba nafikiria suala hilo. lakini kuanzia leo naanza kufikiria kwa undani, kwasababu nilipaswa kusubiria matokeo ya uchaguzi kwanza na mabadiliko yote yatatangazwa yakifuatiwa na uzinduzi.
Hata hivyo, ushindi huo mkubwa ambao ulitarajiwa, umekuwa na ongezeko la kura ikilinganishwa na ushindi wa asilimia 64 mwaka 2012. ambapo mpinzani wa karibu wa Putin milionea, Pavel Grudinin yeye alipata asimilia 12.