Walinzi wa Pwani wa Marekani, wanasema hadi sasa hakuna picha za umma za mabaki ya Nyambizi ya Titan iliyopata ajali na kwamba picha zinazosambaa zilipigwa mwaka wa 2004 na zinaonyesha mabaki ya Titanic yenyewe kwa mfumo bandia.
Usafiri huo uliopata ajali chini ya maji ukiwa umebeba watu watano waliokuwa wakieleka kwenye mabaki ya meli ya Titanic, ilipoteza mawasiliano karibu na eneo la ajali, na kuwaua watu wote watano waliokuwemo ndani ya meli hiyo.
Tumaini la kuwapata wanaume hao watano wakiwa hai lilitoweka saa kadhaa, wakati oksijeni ya meli ilipotarajiwa kuisha na vifusi vilipatikana takriban futi 1,600 (mita 488) kutoka ilipo Meli ya Titanic katika Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini.
“Picha za mabaki yaliyopatikana ya manowari ya #Titan ya kampuni ya Ocean Gate,” inasomeka na moja ya machapisho ya Facebook yaliyoandikwa kwa Kihispania, ambayo yalijumuisha picha mbili zinazoonyesha vitu vya binadamu vilivyofunikwa kwa mchanga na picha nyingine ikiwa na mabaki ya chombo hicho ambazo hazina uhalisia.” walisema.