Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amemfuta kazi mkuu wa shirika la usalama la Ukraine (SBU) na Mwendesha Mashtaka Mkuu, Ivan Bakanov, akitaja visa vingi vya uhaini katika mashirika hayo mawili yenye nguvu.
Rais Zelensky amesema, zaidi ya wafanyakazi 60 wa zamani kwasasa wanafanya kazi dhidi ya Ukraine katika maeneo yanayokaliwa na Urusi.
Amebainisha kuwa, jumla ya kesi 651 za ushirikiano na uhaini zilikuwa zimefunguliwa dhidi ya maafisa wa kutekeleza sheria.
Maafisa waliofutwa kazi ni Ivan Bakanov na Iryna Venediktova ambao bado hawajatoa maoni yoyote.
Katika hotuba yake ya video, Zelensky amesema “Msururu kama huo wa uhalifu dhidi ya misingi ya usalama wa taifa… unazua maswali mazito sana kwa wakuu husika wa mashirika hayo mawili….Kila moja ya maswali haya yatapata jibu sahihi”Rais Zelensky.