Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewaamuru Bodi ya wakandarasi na msajili wa bodi hiyo kumchunguza Mkandarasi ‘Masasi Construction’ na kumfuta kujishughulisha na kazi ya ukandarasi endapo atabainika kuwa hana vigezo.
Rais ameitaka bodi hiyo kutumia sheria namba 17 ya mwaka 1997 ambayo inaruhusu mkandarasi kufungwa hadi miaka mitano.
Masasi Construction ndiye mkandarasai aliyekabidhiwa mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi Mkoani Njombe na kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila kuikamilisha.
Dkt. Magufuli amesema kama hawezi kufanya kazi hiyo akafanye kazi nyingine na si kuchelewesha maendeleo ya wananchi.
”Hauwezi ukapewa kazi halafu kazi huimalizi unatafuta sababu, nchi hii kama huwezi hiyo kazi nenda ukavue samaki, nenda ukatafute kazi nyingine usifanye kazi za kuchelewesha maendeleo ya watanzania, ndio maana tumebadilisha hata sheria zetu kuna sheria hadi za wahujumu uchumi” amesema Rais Magufuli.
Rais ameongezea kuwa haiwezekani taifa hili likawa la majambazi huku wananchi maskini wanahangaika na kuteseka.
Hivyo ametaka mkanfarasi huyo kushughulikiwa na kuwasihi watu wanapopewa kazi kuhakikisha inakamiliaka kwa weledi mkubwa.