Rais wa Kazakhstan, Kassym-Jomart Tokayev amelivunja Bunge la nchi hiyo na kuitangaza siku ya Jumapili Machi 19 kuwa tarehe ya uchaguzi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, imesema Tokayev ameyavunja pia mabunge ya serikali za mitaa nchini humo na kusema anatarajia uchaguzi huo wa mapema utaleta mwamko mpya.
Tokayev, alichaguliwa mwezi Novemba baada ya kushinda asilimia 80 ya kura baada ya uchaguzi uliokosolewa kwa ukosefu wa ushindani.
Aidha, pia wakati huo aliahidi kuiunda Kazakhstan mpya yenye usawa, lakini changamoto za kiuchumi na mienendo ya kidikteta ndiyo mambo yanayoendelea kushuhudiwa katika utawala wake.