Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amesafiri na kuelekea Korea Kusini kwa ajili ya kuhudhuria kikao kati yake na Rais wa nchi hiyo, Moon.
Kim Jong Un amekuwa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kuvuka mpaka na kuingia Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe (Korea) mwaka 1953.
Aidha kwa upande mwingine Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa inatumaini mkutano baina ya viongozi hao utasaidi kukuza amani katika peninsula ya Korea.