Mamia ya watu wameandamana njee ya Bunge la Ufarasansa kupinga kupinga kuongeza kulazimisha mageuzi ya pensheni ambayo yanngeza umri wa kustaafu kwa miaka miwili hadi 64.
Hayo yanajiri baada ya Rais wa Nchi hiyo Emmanuel Macron alilikwepa bunge la Ufaransa na kutumia Mamlaka maalumu ya kikatiba kuongeza umri wa kustaafu
Kabla ya kulikwepa Bunge, Rais Macron, alikuwa ametishia kuivunja taasisi ya kutunga sheria iwapo haitapasisha muswada tata wa kuongeza umri wa kustaafu. Bunge la Ufaransa lilipanga kuupigia kura muswada huo jana Alhamisi.
Sasa serikali ya Ufaransa imetumia mamlaka maalumu kupasisha muswada huo bila kupiga kura bungeni, jambo lililosababisha ghasia na hali ya mchafukoge ambapo wabunge wamemtaka Waziri Mkuu wa Ufaransa, Élisabeth Borne ajiuzulu.
Borne alizomewa na kukejeliwa na Wabunge alipofika Bungeni kutangaza kwamba atatumia Kifungu cha 49.3 cha Katiba, ambacho kinaruhusu hatua ya marekebisho kupitishwa bila ya kupigiwa kura.
Uamuzi huo ulichukuliwa dakika chache kabla ya muswada huo kupigiwa kura katika Bunge la Kitaifa la Ufaransa.
Tangazo hilo limekuja saa chache baada ya Seneti ya Ufaransa, kupitisha muswada huo Alhamisi asubuhi kwa kura 193, jambo ambalo lilitarajiwa kwa kiasi kikubwa ikizingatiwa kuwa maseneti wengi wa kihafidhina wanaunga mkono mpango wa serikali ya Macron.
Kwa mujibu wa mpango huo, umri wa kustaafu nchini Ufaransa umeongezeka kutoka miaka 62 hadi 62. Marekebisho hayo ya umri wa wastaafu yamepingwa vikali na vyama vya wafanyakazi.
Serikali ya Rais Macron imekataa kulegeza kamba na imeendelea kushikilia uamuzi wake wa kuongeza umri wa kustaafu ikitaka kutekelezwa haraka mpango huo wenye utata uliokabiliwa na upinzani mkubwa wa umma.