Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Joseph Pombe Magufuli amefanya uteuzi mwingine wa naibu waziri pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Ambapo amemteua Mbunge wa Songea Mjini Mkoani Ruvuma, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri na Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Aidha Dkt. Ndumbaro amechukua nafasi ya Dkt. Susan Alphonvce Kolimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa na Dkt Mnyepe amechukua nafasi ya Prof, Adolf Mkenda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Uteuzi huo umeanza rasmi leo, Septemba 26, 2018.

 

Jose Mourinho afichua siri ya kutolewa Carabao Cup
Video: Polepole ataja wabunge wengine 3 wa Chadema kuhamia CCM