Hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amekamilisha baraza lake la Mawaziri baada ya jana kutangaza majina ya mawaziri wa wizara nne zilizosalia.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa iliwataja mawaziri hao pamoja na manaibu waziri katika wizara zao kama inavyoonekana hapa.

1.Profesa Jumanne Maghembe -Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

2.Dkt. Philip Mpango – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).

3.Mhandisi Gerson Lwenge – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

4.Dkt. Joyce Ndalichako – Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)

5.Mheshimiwa Hamad Masauni – Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

6.Prof.Makame Mbarawa –Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Askari Polisi Amuua Askari Mwenzake Kwa Risasi na Kisha Kujilipua
Van Gaal awavuruga waandishi na Kuondoka katikati ya Mahojiano