Kocha wa Manchester United, Louis Van Gaal amevurugana na waandishi wa habari katika chumba cha mahojiano na kuamua kuondoka akiwatuhumu kwa kumzushia kuwa tayari amefungashiwa vilago na uongozi wa Klabu hiyo.

Katika mahojiano yake na waandishi wa habari yaliyodumu kwa takribani dakika 4 na sekunde 58 tu, Van Gaal alivishutumu vyombo vya habari kwa kumsababishia usumbufu kwa familia yake huku akivitaka kumuomba radhi kwa taarifa zao kuwa Jose Mourinho tayari ameshafikia hatua ya kuichukua kazi yake.

“Hivi hakuna mtu yeyote kwenye chumba hiki anayejisikia kuniomba msamaha? Hakuna anayejisikia hivyo, ndio maana ninashangaa..! Nadhani tayari nimeshatimuliwa, nimesoma.. nimeshatimuliwa,” aliema Van Gaal.

Meneja huyo aliwaambia waandishi kuwa taarifa zao zimemsababishia wasiwasi kwa ndugu zake ambao wamekuwa wakimpigia simu mara kwa mara kumuuliza ukweli wa habari hizo. Van Gaal mwenye umri wa miaka 64 hakusita kuwaeleza waandishi hao kuwa hapendi kuongea nao ila anafanya hivyo kwa sababu ya sheria tu.

“Hivi mnadhani nataka kuongea na vyombo vya habari sasa hivi? Niko hapa kwa sababu tu ya sheria za Ligi Kuu. Sinabudi kuzungumza nanyi. Lakini ninaona wakati ninapozungumza kitu na mnavyoyatumia maneno yangu kwa namna yenu,” alisema kocha huyo.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger pia aliwakosoa waandishi wa habari na kueleza kuwa walichomfanyia Van Gaal ni kumkosea heshima.

Van Gaal na Arsene Wenger

Van Gaal na Arsene Wenger

 

Rais Magufuli amalizia Safu ya Mawaziri wake, Awatangaza waliosalia
Waongezewa Kifungo Baada ya Kushuti Video ya Rap Wakiwa Gerezani, itazame hapa