Rais John Magufuli, leo amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26 wa Tanzania Bara na kuipangua safu ya wakuu wa Mikoa walioachwa na mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete.

Katika uteuzi huo uliotangazwa leo na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe Ikulu Jijini Dar es salaam, wateule 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

Katika safu hiyo, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ameukwaa Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kusifiwa na Rais John Magufuli kwa utendaji wake katika wilaya yake. Makala amechukua nafasi ya Said Meck Sadick ambaye amehamishiwa Mkoa wa Kilimanjaro.

Wateule wote wanatarajiwa kuapishwa Jumanne, Machi 15 mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi.

Hawa ndio wakuu wa Mikoa waliotangazwa: 

  1. Mh. Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
  2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga – Mkuu wa Mkoa wa Geita.
  3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu – Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
  4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga – Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
  5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga – Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
  6. Mh. Godfrey Zambi – Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
  7. Dkt. Steven Kebwe – Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven – Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
  9. Mh. Anna Malecela Kilango – Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  10. Mhandisi Methew Mtigumwe – Mkuu wa Mkoa wa Singida.
  11. Mh. Antony Mataka – Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
  12. Mh. Aggrey Mwanri – Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
  13. Mh. Martine Shigela – Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  14. Mh. Jordan Mungire Rugimbana – Mkuu wa Mkoa Dodoma.
  15. Mh. Said Meck Sadick – Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
  16. Mh. Magesa Mulongo – Mkuu wa Mkoa Mara.
  17. Mh. Amos Gabriel Makalla – Mkuu wa Mkoa Mbeya.
  18. Mh. John Vianey Mongella – Mkuu wa Mkoa Mwanza.
  19. Mh. Daudi Felix Ntibenda – Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  20. Mh. Amina Juma Masenza – Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
  21. Mh. Joel Nkaya Bendera – Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
  22. Mh. Halima Omary Dendegu – Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
  23. Dkt. Rehema Nchimbi – Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
  24. Mhandisi Evarist Ndikilo – Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
  25. Mh. Said Thabit Mwambungu – Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
  26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa – Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).

Mama Terry anavyoingiza Mamilioni kwa 'PhD ya Ngono'
Chadema yapata Katibu Mkuu Mpya, mfahamu hapa na sifa zake