Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John magufuli, amsema siri ya kuteua wanajeshi wengi Serikalini ni kutaka kuingiza Serikali kwenye nidhamu kutoka kwa wanajeshi hao.

Magufuli alisema anataka kuichukua nidhamu iliyopo jeshini na kuingiza Serikalini kwa sababu alipoingia  madarakani alikuta mambo mengi yako hovyo.

Aliyasema hayo wakati wa chakula cha mchana na wanajeshi wapya wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) mwishoni mwa wiki alipo watunuku Kamisheni katika Viwanja vya Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo alisema imani yake kwa wanajeshi ndiyo inayomfanya awape kipaumbele.

“Saa nyingine hata katika uteuzi wangu huwa najisahau kila nafasi inapotokea nateua mwanajeshi,lakini nafanya hivyo kwa sababu nina imani kubwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa sababu ukiwapa jukumu wanafanya kwa ujasiri mkubwa na kwa moyo wote na kwa kuitanguliza Tanzania kwanza.”alisema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli aliwataka wanajeshi kutembea kifua mbele wakijua yuko nao na anachotaka ni kuchukua nidhamu yao na kuingiza Serikalini.

 

 

Video: Kikwete asimulia alivyopewa kuku na mzee Xavery Pinda, 'alikuwa mtu mwema sana'
Msajili atetea uamuzi wa taasisi za umma kuweka fedha ‘fixed Deposit Account’