Rais wa nchi ya falme za kiaarabu Sheikh Khalifa bin Zayed Al-Nahyan, amefariki akiwa na miaka 73 baada ya kuugua kwa muda mrefu, kifo chake kimedhibitishwa na kituo cha habari kinachomilikiwa na serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu.
Kufuatia kifo hicho Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za Pole na kuungana na Jumuiya ya watu wa falme za kiarabu Katika kipindi hiki cha majonzi akimuelezea Sheikh Nahyan kama kiongozi mahiri.
Nafasi ya rais Sheikh Khalifa inatarajiwa kujazwa na kaka yake mfalme Mohammed bin Zayed, ambaye tayari anaonekana kuwa kiongozi wa UAE, na sababu ya kifo chake haijatajwa.
Siku 40 za maombolezi zimetangazwa, ambapo bendera zitaperushwa nusu mlingoti huku wafanyikazi wa umma na wale wa sekta za kibnafsi wakitakiwa kupumzika kwa siku za kwanza tatu kama ishara ya kuonyesha heshima kwa hayati Sheikh Khalifa.
Sheikh Khalifa, aliingia madarakani kama kiongozi wa pili wa nchi hiyo ya miliki za kiarabu novemba 2004 akichukua nafasi ya babake kama kiongozi wa 16 wa Abu Dhabi.
Khalifa, hajaonekana katika umma tangu mwaka wa 2014 alipofanyiwa upasuaji baada ya kupooza japokuwa mchango wake mkubwa katika uwongozi uliendelea kuonekana.