Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 18,2021 amezindua kiwanda cha nyama cha Eliya Food Overseas kilichopo Longido mkoani Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikata utepe kufungua kiwanda cha Nyama cha Eliya Food Overseas kilichopo Longido Arusha

Aidha, Rais Samia amezindua mradi mkubwa wa maji Longido utakaowanufaisha wananchi zaidi ya 13,000, ambapo mradi huo umegharimu bilioni 4.5 na utapeleka maji katika Mji wa Namanga na kuwaondolea kero ya maji wananchi wa mji huo.

Sambamba na hayo pia Rais Samia amesisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Serikali kufanya kazi kwa nidhamu na bidii ili kusimamia maendeleo ya Taifa

Aidha Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wakazi wa Longido kujitokeza kwa ajili ya zoezi la kuhesabiwa linalotarajia kufanyika mwakani nchini Tanzania.

Mmarekani mweusi wa kwanza kuwa waziri masuala ya kigeni afariki dunia
Tanzania, Kenya kumaliza vikwazo vya kiutawala Disemba