Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Jumapili Septemba 12, 2021 atapokea taarifa juu ya maandalizi yanavyokwenda na juhudi mbalimbali katika kurekebisha soko la Kariakoo.

Ameyasema hayo leo Septemba 12, 2021 wakati akizungumza na vyombo vya habari ambapo ameeleza kuwa lengo la serikali ni kulifanya soko la Kariakoo kuwa la kimataifa kama masoko mengine duniani.

”Wiki hii kumekuwa na mjadala juu ya Soko la Kariakoo naomba kuwaambia kwamba maandalizi ya kulikarabati soko hilo yanaendelea, lengo la serikali ni kuhakikisha baada ya ajali ile ya moto, soko la Kariakoo lirudishwe katika sura ya soko la kimataifa,” amesema Msigwa

”lengo letu sasa ni kwamba soko la kariakoo litakaporudi liwe ni la kimataifa, soko ambalo linaendeshwa kama masoko mengine duniani, kama ni biashara saa 24 zifanyike mazingira yawe salama”.amesema Msigwa

Naibu Waziri Ummy : Akemea ukatili kwa vijana
Waziri Bashungwa : Serikali kuendelea kuwainua wasanii