Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi na mkewe Isaura wamekutwa na maambukizi ya virusi vya Uviko-19baada ya kufanya vipimo kutokana na shughuli nyingi ambazo walizifanya wiki chache zilizopita.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Rais imesema kuwa Rais Nyusi na mkewe wamejitenga baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa huo.

Kumekuwa na ongezeko la virusi vya corona katika siku za hivi karibuni nchini Msumbiji, ambapo watu 193,000 wanaougua Covid-19, huku vifo 2,031 vikirekodiwa.

Rais Samia afanya uteuzi
Gari linalotumia umeme pekee lazinduliwa