Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, amemteua Dkt Baghayo Abdallah Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania TIRA, Dkt Saqware ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania TIA.

Aidha Rais Samia amemteua Charles Jackson Itembe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalum la Mauzo ya Nje EPZA. kabla ya uteuzi Itembe alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania (Azania Bank Limited).

Ernest Maduhu Mchanga ameteuliwa kuwa Katibu wa Tume ya pamoja ya Fedha JFC, Mchanga ni Katibu Msaidizi Fedha na Utawala Tume ya Pamoja ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.

Uteuzi huu umeanza Januari 1, 2021

CCM wafunguka maombi ya Ndugai kwa Rais, Watanzania
Rais wa Msumbiji , mkewe wakutwa na Covid 19