Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amemaliza ziara yake nchini Marekani, ambapo amesema kuwa hakuenda kumshawishi rais wa nchi hiyo kuhusu kubadili mtazamo wake katika mpango wa nyuklia dhidi ya Iran.
Trump anapinga makubaliano ya kimataifa yaliyofikiwa mwaka 2015, yanayolenga kuidhibiti Iran kuhusiana na mpango wake wa Nyuklia.
“Sina taarifa zozote za ndani kuhusiana na uamuzi wa rais Trump kuhusu mkataba wa nyuklia wa Iran (JCPOA). Kufuatia kile kinachodaiwa kwamba, nilimsikiliza alichosema kwamba inaonekana hana nia ya kuutetea mpango huo,”amesema Rais Macron
Macron amesema kuwa hakuwa anajaribu kubadili msimamo wa rais Trump kama atajitoa katika makubaliano, lakini badala yake atafanya kila linalowezekana kuhakikisha mpango wa nyuklia wa Iran unaendelea kuzuiwa.
Hata hivyo, Macron amesema kuwa jambo analolifanya ni kuhamasisha mkataba huo unakuwa wenye tija, katika kukabiliana na kuthibiti shughuli za kinyukilia za Iran, na kuweka mikakati ya Kidiplomasia ili kuhakikisha uamuzi wowote utakaochukuliwa na rais Trump usiwaathiri.