Mwanasheria mkuu wa New York amemtaka Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump pamoja na wanawe wawili kufika ofisini kwake kutoa ushahidi katika uchunguzi kuhusiana na biashara za familia hiyo.

Kwa mujibu wa Gazeti la Washington Post nchini humo limeripoti kuwa mwezi Disemba mwaka jana mwanasheria huyo mkuu Letitia James alimuomba Trump kwenda mwenyewe ofisini kwake ifikapo Januari 7.

Hii ni mara ya kwanza kwa wachunguzi hao kusema watawaita na watoto wakubwa wa Trump, Donald Trump Jr na Ivanka kutoa ushahidi chini ya kiapo.

James anachunguza iwapo makampuni ya Trump yalivunja sheria yaliporipoti thamani ya mali zake ili kupata nafuu zaidi ya kodi na benki.

Hata hivyo wakili wa Trump Alina Habba amesema watakatia rufaa mwito huo.

Magwiji wafufua European Super League
CCM wafunguka maombi ya Ndugai kwa Rais, Watanzania