Klabu za Real Madrid, FC Barcelona na Juventus wameripotiwa kufanya mazungumzo mapya kuhusu kufufua Michuano ya European Super League, ikiwa ni miezi minane tangu pendekezo hilo kuzinduliwa.

Wazo hilo lilisababisha utata katika Jumuiya ya Soka Barani Ulaya na klabu nyingine kujiondoa, lakini Real Madrid, FC Barcelona na Juventus zimeshikilia msimamo wa wazo la kuanzisha Michuano hiyo.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Mirror, maofisa wakuu kutoka kwa klabu tatu zinazohusika wote wamekutana na wako tayari kuzindua tena pendekezo lao la Super League.

Florentino Perez wa Real Madrid, Joan Laporta wa FC Barcelona na Andrea Agnelli wa Juventus wanadaiwa kukubaliana, mnamo Oktoba, juu ya mabadiliko matano muhimu ya kanuni za mashindano yaliyopendekezwa katika jaribio lao la kwanza la kufufua Super League.

Pendekezo hilo la mwezi wa Aprili lilizua taharuki kutoka kwa mashabiki, haswa Uingereza, na kwa hivyo Real Madrid, Barcelona na Juventus waliajiri kampuni kubwa ya Uhusiano wa Umma yenye makao yake jijini London ili kusaidia kupata kura za mashabiki kutoka kwa klabu za Ligi Kuu England.

Kocha Pablo atangaza njaa Mapinduzi Cup
Rais wa zamani wa Marekani kuchunguzwa