Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameshtumu ghasia za hivi karibuni juu ya mashambulizi dhidi ya wageni na kutoa wito kwa taasisi za kiusalama kuwakamata wanaotekeleza vitendo hivyo.
Hivyo Waziri wa Mambo ya kigeni nchini Afrika Kusini ameitisha mkutano wa dharura na mabalozi kufuatia mashambulizi dhidi ya wageni mjini Durban.
Mapema Jumatatu watu 3 wamefariki dunia kufuatia maandamano yanayolenga maduka mengi ambayo yanamilikiwa na wageni, ambapo takribani watu 100 walishambulia maduka ya vyakula siku ya Jumapili na Jumatau pamoja na kuiba baadi ya bidhaa na kuchoma moto maduka hayo .
Chanzo cha vurugu hizo kimetajwa kuwa ni raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kudaiwa kuchukua kazi za raia wa taifa hilo na kuwafanya wabaki bila kazi kwani 72% ya raia wa nchi hiyo kwa mwaka 2018 wanasemekana kukosa ajira.
Kufuatia vurugu hizo zinazoendelea zimepelekea takribani watu 50 kutafuta hifadhi katika kituo kimoja cha polisi wakati.
Amesema kuwa ghasia hizo, ambazo zimekuwa zikiwalenga raia wa Malawi na raia wengi wa Afrika katika jimbo la Kwazulu Natal ni swala la kujutia hususan katika mkesha wa siku ya mwezi wa uhuru ambapo taifa hilo linaadhimisha miaka 25 tangu uchaguzi wa kidemokrasia nchini humo.
Aidha Mashambulizi dhidi ya wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika sio jambo geni nchini Afrika kusini.
Mwaka 2015, ghasia katika miji ya Johannesburg na Durban zilisababisha mauaji ya watu saba baada ya wahamiaji kuwindwa na kushambuliawa na magenge.
Afrika kusini ilikumbwa na ghasia mbaya zaidi dhidi ya wageni mwaka 2008 wakati ambapo zaidi ya watu 60 waliuawa.