Pamoja na mambo kwenda mrama kwenye kikosi cha Chelsea, kufuatia matokeo mabovu yanayoonekana, kiungo kutoka nchini Brazil Ramires Santos do Nascimento, amekubali kujitia kitanzi cha kuendelea kubaki Stamford Bridge.

Ramires, amekubaliana na hali hiyo, kwa kuafiki kusaini mkataba wa miaka mitatu ambao utafikia kikomo mwezi June mwaka 2019.

Hali hiyo inatafsiriwa kama hatua ya kumbeba meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho, ambaye kwa sasa hana budi kurekebisha hadhi ya klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London.

Tayari Ramires alikua ameshaanza kuhusishwa na mipango ya kutaka kusajiliwa na klabu buingwa nchini Italia, Juventus, lakini bado hakuonyesha tamaa ya kuondoka Stamford Bridge.

Ramires amekua mmoja wa wachezaji wanaoonyesha kujituma vilivyo kwenye kiksoi cha Chelsea, na wakati mwingine amekua akitumia uwezo binafsi pale inapohitajika kufanya hivyo ili kufikia lengo la ushindi.

Ramires, alisajiliwana Chelsea, mwaka 2010 akitokea kwenye klabu ya Benfica ya nchini Ureno.

Wenger Kuwakosa Walcott, Chamberlain
Dkt. Magufuli, Samia Wakabidhiwa Vyeti Vya Ushindi