Washambuliaji wa Arsenal Theo Walcott pamoja na Alex Oxlade-Chamberlain wanatarajiwa kurejea uwanjani mara baada ya michezo ya kimataifa ambayo imepangwa kuchezwa mapema mwezi ujao.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha taarifa hizo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliokua unazungumzia mchezo wa ligi ya nchini England, utakaochezwa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Swansea City.

Iliwachukua dakika 20, wachezaji hao kutolewa nje ya uwanja, wakati wa mchezo wa kombe la ligi uliochezwa siku ya jumanne ambapo Arsenal walikubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Sheffield Wednesday.

Oxlade-Chamberlain, alishindwa kuendelea na mchezo huo kufutia maumivu ya misulu ya paja na Walcott, aliyechukua nafasi yake alitumia muda wa dakika chache kabla ya kupata maumivu ya kiazi cha mguu.

Wenger, amesema wachezaji hao watakosa michezo mitatu kuanzia mchezo wa mwishoni mwa juma hili, hali ambayo inadhihirisha wazi, hawatokuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya England ambacho kitacheza michezo ya kirafiki mwezi ujao.

Hata hivyo mzee huyo kutoka nchini Ufaransa, amewatoa hofu mashabiki wa Arsenal, kwa kusema hakuna lililoharibika zaidi ya kutambua ana wachezaji wengine ambao wana uwezo wa kuziba nafasi za Theo Walcott pamoja na Alex Oxlade-Chamberlain.

Malinzi Ampongeza John Pombe Magufuli
Ramires Akubali Kumuokoa Mourinho