Fedha ya Afrika Kusini, rand, inaendelea kuporomoka thamani kwa kasi baada ya Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kumfukuza kazi waziri wa fedha mwenye uzoefu mkubwa, Pravin Gordhan.

Aidha, Zuma alitangaza uamuzi huo Alhamis hii kuwa anamuondoa Gordhan madarakani pamoja na mawaziri wengine. Wawekezaji walikuwa wameshaanza kuhofia kuwa Zuma angemtimua waziri huyo baada ya Jumatatu kumuamuru asitishe mikutano yake na wawekezaji wa nje.

Hatua hiyo pia ilikuwa ni dhoruba kwa rand ambayo sasa imeshuka thamani yake kwa asilimia 8. Wachambuzi walionya mapema wiki hii kuwa kumuondoa Gordhan na mawaziri wengine kutaleta madhara makubwa ambayo yatasababisha uchumi wa nchi hiyo kuyumba.

Hata hivyo, Gordhan amekuwa waziri wa fedha kwa muda mrefu kuanzia mwaka 2009 hadi 2014 na kurudi tena December 2015. Zuma amemteua Malusi Gigaba aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani kushika nafasi hiyo.

Ahukumiwa Miaka Mitatu Jela kwa Kughushi Cheti
Zanzibar kutegua kitendawili cha tatizo la umeme