Rapa mkubwa wa Kenya, Khaligraph Jones ameonesha kumsikitikia kiongozi wa La Familia, Chidi Benz ambaye hivi karibuni alijitokeza hadharani akiomba msaada baada ya kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Khaligraph Jones

Khaligraph amekiambia kipindi the Playlist cha 100.5 Times Fm kuwa yeye alikuwa shabiki mkubwa wa Chidi Benz tangu zamani na kwamba alisikitishwa na taarifa za matatizo yaliyomsibu kutokana na matumizi ya dawa hizo.

Kadhalika, Rapa huyo ambaye hivi sasa ni tishio kwenye msululu wa rap Afrika Mashariki alimshukuru sana Babu Tale kwa msaada wake kwa Chidi Benz.

“Babu Tale nilikuwa simfahamu zaidi ya kujua ni meneja wa Diamond, lakini si ndio yule aliyempeleka Chidi Benz Sober House… amefanya jambo jema sana nampongeza, Mungu atamsaidia,” alisema Khaligraph.

Katika hatua nyingine, Khaligraph ambaye anajipanga kuachia album yake mpya itakayokuwa bomu kubwa kwenye game amesema kuwa yuko katika mpango wa kufanya wimbo na rapa kutoka Ghana, Sarkodie.

Tyson ataka Manny Pacquiao apigwe marufuku kucheza masumbwi
CUF yaivaa China baaa ya kuusifia uchaguzi wa marudio na kutoa msaada