Bingwa wa dunia wa zamani wa ndondi, Mike ‘Iron’ Tyson ametaka vyombo vyenye mamlaka, kumpiga marufuku bondia kutoka Ufilipino, Manny Pacquiao kushiriki mchezo wa masumbwi.

Manny Pacquiao

Tyson ametoa maoni hayo alipofanya mahojiano na TMZ akieleza kuwa sababu ya kutaka hatua hizo zichukuliwe ni tamko la Pacquiao kudai kuwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanazidiwa na wanyama.

Pacquiao pia ambaye ni mtu aliyeishika dini ya Kikristo aliwahi kupost Instagram maandiko ya Biblia yanayoeleza kuwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja wanapaswa kufa.

Tyson amesema kuwa kauli za Pacquiao zinaumiza hisia za watu wengine na kuwakosea heshima ingawa mtazamo wake unaungwa mkono na watu wa imani ya dini yake.

 

Mapenzi: Mrembo alipia Bango katikati ya jiji akitangaza kuwa bikira, adai anasaka ‘tendo’ kabla hajafa
Rapa Mkubwa Kenya Amsikitikia Chidi Benz