Klabu ya Simba SC imetawazwa kuwa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo.

Simba SC wametetea taji lao, baada ya kuifunga Coastal Union ya Tanga mabao 2-0, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Mabao ya Simba SC yamepachikwa kimiani na washambuliaji John Bocco na Criss Mushimba Mugalu katika kipindi cha kwanza.

Ushindi huo unaifanya Simba SC kufikisha alama 79, baada ya kucheza michezo 32, sawa na timu zote za Ligi Kuu msimu huu 2020/21.

Ni Rasmi alama za Simba SC haziwezi kufikiwa na timu yoyote shiriki kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu huu, ni dhahir wanatawazwa kuwa Mabingwa 2020/21.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 12, 2021
Hii ndo faida ya ithibati