Aliyekua beki wa Man Utd, Rio Ferdinand amewanyima nafasi Arsenal ya kusonga mbele katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, kufuatia ugumu wa mchezo wao wa mkondo wa pili wa hatua ya 16 bora wa ligi ya mabingwa barani humo, dhidi ya FC Barcelona.

Ferdinand ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za West Ham Utd, Leeds Utd pamoja na Queens Park Rangers, amesema ni vigumu kuamini kama Arsenal watakuwa na nafasi ya kusonga mbele, kutokana na mazingira wanayokwenda kukutana nayo uwanja wa ugenini.

Beki huyo ambaye kwa sasa ameamua kutundika daruga, amesisitiza kwamba, kinachomuaminisha juu ya suala hilo ni kwamba, hakutokua na mabadiliko ya matokeo katika mchezo wa hii leo, kutokana na mwenendo wa kikosi cha Arsene Wenger katika michezo ya hivi karibuni ambao umekua mbovu tofauti na ilivyokua mwanzoni mwa msimu huu.

Amesema haoni kama kuna morari kwa wachezaji wa Arsenal, ambao walipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu, lakini mwihowe wameshindwa kushinda hata michezo ambayo waliaminiwa wangefanya makubwa.

Amedai kwamba, Arsenal kwenda ugenini wakiwa na deni la kufungwa mabao mawili kwa sifuri, kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza hilo ni kosa kubwa sana kwao, ambalo haliwezi kufutika kirahisi katika uwanja wa Camp Nou.

Arsenal wanakwenda ugenini hii leo, huku wanyeji wao wakiwa wanajidai kuwa na safu hatari ya ushambuliaji inayoundwa na Lionel Messi, Luis Suarez pamoja na Neymar ambayo tayari kwa msimu huu imeshafunga mabao 103.

Main Image

Arsenal endapo watahitaji kusonga mbele katika michuano hiyo, watatakiwa kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri na kuendelea, lakini kinyume na hapo itakua ni kazi bure.

Aggrey: Nimerejea Kuisadia Azam FC
Thomas Mashali Autamani Ubingwa Wa Francis Cheka