Wakali wa michano, Roma na Stamina wanaounda kundi la ‘Rostam’ wamesema kuwa moja kati ya sababu zinazoweza kuvunja kundi lao ni ‘michepuko’.

‘Rostam’ ambao wamejijengea sifa kwa ‘makamuzi’ yao kila wanapokuwa jukwaani wamesema kuwa wamejiwekea masharti ya kutojihusisha na michepuko wanaposafiri kwenda kwenye matamasha mikoani, hivyo ikitokea mmoja akavunja sharti hilo atakuwa ameua kundi.

Roma ambaye ni mwanandoa na baba wa mtoto mmoja amesema kuwa utaratibu huo wameuweka ili pamoja na mambo mengine waweze kuwalinda wenzi wao wanapokuwa wamesafiri kikazi hususan mikoani.

“Ni vigezo na mikakati ya kundi tuliyojiwekea. Unajua mimi nimeoa na Stamina hivi punde anaingia huko, yupo serious kila siku ananitumia jumbe za mchango. Kwahiyo, tumeshajiwekea hivyo, mtu yeyote akichukua demu (msichana) mkoani kundi linavunjika hapohapo,” Roma aliiambia XXL ya Clouds FM.

 

Naye Stamina alieleza kuwa ingawa sharti hilo ni gumu kutekelezeka kwa sababu ya mambo mengi yaliyoko mikoani, hawana bundi kutekeleza ili kulinda afya zao.

Roma na Stamina (Rostam) wanaendeleza ubabe kwenye vyombo vya habari, mitaani na kwenye matamasha mbalimbali kupitia wimbo wao ‘Hivi au Vile’.

Chama cha CCK chapanga kufanya mkutano mkuu Ikulu
Ahukumiwa mwaka mmoja jela kwa kumkashifu Rais Magufuli WhatsApp