Meneja wa klabu ya Southampton, Ronald Koeman amesisitiza kuwa tayari kusiani mkataba mpya wa kuendelea kufanya kazi huko St Marries Stadium.

Koeman, ametoa msisitizo huo ikiwa ni baada ya juma moja kupita ambapo ilisemekana huenda angekubali kurejea nyumbani kwao Uholanzi, na kuchukua jukumu la kuifundisha timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo imeshindwa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya.

Chama cha soka nchini Uholanzi, kilithubutu kulihusisha jina la meneja huyo kwenye orodha ya wanaofikiriwa kuchukua mikoba ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya hiyo kwa sasa Danny Blind, ambaye ameonekana kushindwa kufikia malengo aliyokua amepangiwa.

Katika mchakato huo Komen alionekana kuwa chaguo la wengi, na ndipo taarifa za kupigiwa chapuo la kupewa ajira ya kuwa kocha mkuu zilipoanza kusikika kupitia vyombo vya habari.

Lakini pamoja na yote hayo, Komen ameonyesha kuhitaji kufanya kazi upande wa klabu, kutokana na kauli yake ya kuwa tayari kusaini mkataba mpya wa klabu ya Southampton ambayo ilimuajiri mwanzoni mwa msimu uliopita.

Mkataba wa sasa wa meneja huyo kutoka nchini Uholanzi umebakisha muda wa miezi 18 (mwaka mmoja na nusu) ikiwa ni sehemu ya miaka mitatu ambayo imeainishwa kwenye makubaliano ya awali.

Kikosi cha The Saint, kimeonyesha kuwa na mustakabali mzuri wa ushindani katika ligi ya nchini England, hali ambayo imeendelea kuwavutia viongozi wa Southampton kutaka kufanya kazi ya Koeman.

Mourinho: Sijafurahishwa Na Ajira Ya Klopp
Herrera Awatishia Nyau Schweinsteiger Na Carrick