Meneja wa klabu ya Chelsea, ameonyesha kusikitishwa na hatua ya klabu ya Liverpool kumuajiri Jurgen Klopp, kama mbadala wa Brendan Rodgers ambaye alitimuliwa kazi klabuni hapo mwanzoni mwa mwezi huu.

Mourinho, ameonyesha kuchukizwa huko, kwa kuhofia huenda historia ya meneja huyo kutoka nchini Ujerumani ikachafuliwa na utaratibu uliojengeka huko Anfield wa kushindwa kukaa na meneja mmoja kwa kipindi kirefu.

Amesema inauma kuona Brendan Rodgers anaondoka Liverpool, ili hali alionyesha kuimudu timu ya majogoo wa jiji, lakini uharaka wa viongozi wa klabu hiyo ulikua kikwazo kwa meneja huyo kutoka Ireland ya kaskazini.

Mourinho, anahofia jambo hilo kumtokea Klopp, ambaye ana historia nzuri katika soka la barani Ulaya, kufuatia mchango mkubwa alioutoa kwenye klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani.

Amesema jambo kubwa ni kumtakia kila la kheri Klopp, ili aweze kufikia lengo linalokusudiwa na viongozi wa Liverpool, na amesisitiza hatofurahishwa pale itakapotokea mambo kwenda kinyume na matarajio ya watu wa klabu hiyo ya mjini Liverpool.

Tayari Klopp ameshaonja joto ya ligi ya nchini England kwa kukishuhudia kikosi chake kikipambana mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Spurs, na kuambulia matokeo ya sare ya bila kufungana.

Mabomu Yakutwa Kwenye Gari La Mbunge Wa Chadema
Ronald Koeman Kubaki St Marries